RUTO: UN IFANYIWE MAGEUZI KUZUIA MIGOGORO
Rais William Ruto ameshinikiza mageuzi katika baraza la usalama la umoja wa Mataifa ili kukabili changamoto zinazoibuka.
Kwa mujibu wa Rais Ruto, mfumo uliopo kwa sasa umeshindwa kukabiliana na migogoro inayoibuka hususan suala la mabadiliko ya tabia nchi, kutokuwa na usawa na madeni.
Akizungumza katika mkutano wa marais jijini New York ulioangazia mustakabali wa mataifa wanachama, Ruto amesema mageuzi yatazuia migogoro ya kimataifa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































