IPOA: WANAHABARI MKO SALAMA

Afisa mkuu mtendaji wa mamlaka huru ya kuangazia mienendo ya maafisa wa polisi IPOA Elema Halake ametoa hakikisho la usalama kwa mwanahabari wa Nakuru Catherine Wanjeri aliyejeruhiwa kwa kupigwa risasi wakati wa maandamano ya kupinga mzigo wa ushuru.
Akizungumza katika warsha ya kuwahamasisha wanahabari kuhusu usalama wao jijini Nakuru, Halake amesema tayari IPOA imeanzisha uchunguzi baada ya kuibuka madai kwamba mwanahabari huyo anatishiwa.
Kwa mujibu wa mwanahabari huyo, amekuwa akishinikizwa kuondoa kesi mahakamani.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa