#Sports

HATUJALIPWA PESA ZETU

Baadhi ya wanariadha ambao walishiriki mbio za Eldoret city marathon zilizofanyika April 21 mwaka huu mjini eldoret wamejitokeza na kudai kuwa hawajapokea malipo yeyote ambayo walifaa kulipwa.

Kulingana na wanariadha hao, waandalizi wa mbio hizo walikuwa wamewahidi wanariadha hao kuwa wangefaa kulipwa kufikia tarehe 26 juni mwaka huu lakini hadi sasa hawajapokea malipo yeyote licha ya kupeana nambari za akaunti zao za benki na kuafiki matakwa yote hitajika.

Wakiongea na wanahabari mjini iten, wanariadha hao wametaka wafadhili na waandalizi wa mbio hizo hasa wizara ya michezo kuwalipa malipo yao kwa kuwa wanapitia changamoto nyingi.

Kwa upande wake kocha Hillary Cheruiyot ametaka serikali kuhakikisha kuwa wanariadha hao wanalipwa la sivyo wataandamana kushinikiza malipo ya wanaridha.

Imetayarishwa na Nelson Andati

HATUJALIPWA PESA ZETU

SABABU ZA KUKATALIWA KWA SOI KUWA WAZIRI

HATUJALIPWA PESA ZETU

WACHEZAJI 22 WAREJEA NDANI YA CITY

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *