WANGA; RAILA BADO NDIYE KIONGOZI WA AZIMIO

Gavana wa kaunti ya Homabay Gladys Wanga na mbunge wa kasipul Charles Ongondo Were wamewasuta badhi ya viongozi katika mrengo wa azimio kwa madai ya kupindua uongozi wa kinara wa chama cha ODM Raila Odinga katika muungano huo.
Wanga amekashifu viongozi hao akitaja hatua ya wao kusema kwamba Kalonzo ndiye atakayeongoza mrengo huo kuwa mapinduzi dhidi ya Raila Odinga.
Imetayarishwa na Janice Marete