TER STEGEN

Kipa wa Barcelona, Marc-Andre ter Stegen atafanyiwa upasuaji wa mshipa wa goti uliochanika, huku nahodha huyo wa klabu hiyo akitarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa salio la msimu huu.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 32 alitolewa nje kwa machela baada ya kuanguka vibaya wakati timu yake iliposhinda 5-1 dhidi ya Villarreal siku ya Jumapili.
Ter Stegen, ambaye alikosolewa baada ya kufanya makosa katika kichapo cha 2-1 cha Barcelona kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Monaco siku ya Alhamisi, alipata jeraha hilo kabla ya kipindi cha mapumziko katika uwanja wa Villarreal Estadio de la Ceramica.
Inaki Pena alichukua nafasi ya Ter Stegen na anatazamiwa kuchukua nafasi ya Mjerumani huyo Kwa mechi zijazo, ingawa Barcelona wanaweza kutafuta mbadala wake.
Flick alisema ni mapema sana kutoa maoni juu ya suala hilo.
Ter Stegen alianza mechi mbili za Ligi ya Mataifa akiiwakilisha Ujerumani mwezi Septemba baada ya mkongwe wa Bayern Munich Manuel Neuer kustaafu kucheza kimataifa mwezi Agosti.
Imetayarishwa na Nelson Andati