“TUSHIRIKIANE KUMALIZA MAAMBUKIZI YA MARATHI” KATIBU WA AFYA MARY MUTHONI
Katibu wa idara ya afya ya umma Mary Muthoni amewataka wakenya kushirikiana na wahudumu wa afya wa kijamii ili kudhibiti maambukizi ya magonjwa mbali mbali kusambaa.
Akizungumza katika kaunti ya Kisumu Muthoni amesema wahudumu hao wa kijamii wamepokea mafunzo muhimu na vifaa vya kuwawezesha kutoa huduma za kiafya katika kutibu marathi mbali mbali katika jamii.
Muthoni amesema serikali nimewasajili wahudumu wa afya ya kijamii elfu 107 ambapo wanatakiwa kushughulikia familia 100 kila mmoja.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































