#Local News

MCHAKATO WA KIDIJITALI WA UNUNUZI UTAOKOA ASILIMIA 30 YA RASLIMALI ZA UNUNUZI

Serikali inatarajiwa kuokoa asilimia 30 ya raslimali za ununzi wa umma mchakato wa ununuzi utakapowekwa kikamilifu kuwa wa kidijitali ifikiapo Januari mwaka wa 2025.

Kwa mujibu wa taasisi ya ugavi na usimamizi mchakato huo unatarajiwa kupunguza visa vya ulaghai katika sekta hiyo.

Mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo Kenneth Matiba kwa upande wake amesema kuwa mchakato huo utakuwa wa kiotomatiki bila karatasi na unatarajiwa kuharakisha mchakato wa ununuzi katika mashirika yote ya serikali ya kitaifa na kaunti.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *