KUPPET YAIKABA TSC
Muungano wa kutetea maslahi ya walimu wa shule za upili na vyuo vya kadri KUPPET umeitaka tume ya kuwaajiri walimu TSC kutatua changamoto wanazopitia walimu wa shule za sekondari msingi JSS, ukiwemo ukosefu wa vifaa muhimu.
Wakizungumza katika eneo la Gisambai kaunti ya Vihiga, viongozi wa KUPPET wakiongozwa na mwenyekiti Omboko Milemba na kaimu katibu mkuu Moses Nthurima, wamesema ukosefu wa vifaa hivyo umeathiri utendakazi waw alimu hao.
Wameahidi vile vile kuishinikiza serikali kuwapandisha vyeo walimu waliohitimu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































