SERIKALI YA MAREKANI YAHOFIA ONGEZEKO LA UDANGANYIFU WA HATI ZA ARDHI NCHINI KENYA
Kwa mara ya kwanza katika ripoti rasmi ya biashara Mwakilishi wa Biashara wa Marekani ameelezea wasiwasi kuhusu ongezeko la udanganyifu wa hati za ardhi nchini Kenya, na kutahadharisha kwamba wawekezaji wanajiingiza kwenye hatari ya kulaghaiwa kupitia hatimiliki ghushi za ardhi zilizotolewa mara mbili, hasa wanapokuwa wanakodisha ardhi ambayo haijawahi kuendelezwa.
Hii ni kutokana na udanganyifu unaohusisha mawakala wasiokuwa waaminifu na baadhi ya maafisa wa serikali.
Udanganyifu huu umeigharimu benki na biashara mabilioni ya fedha kupitia kesi mahakamani na dhamana za uongo, na kuleta hasara kubwa katika sekta ya fedha.
Vile vile maendeleo yamekuwa polepole kutokana na upinzani kutoka kwa magenge ya wahalifu na baadhi ya mawakili.
Wizara ya Ardhi imetangaza mipango ya mageuzi, ikiwa ni pamoja na uhifadhi wa kidijitali wa rekodi za ardhi, ili kupunguza ulaghai huu
Imetayarishwa na Mercy Asami
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































