MAFUNZO KWA MAKOCHA
Makocha 30 kutoka kaunti ya Mombasa wameanza mafunzo ya kuhitimu na cheti cha CAF D na ambacho ndio cheti cha chini kabisa na cha mwanzo katika kusomea ukufunzi huku mafunzo hayo yakiendelea katika ukumbi wa shule ya Ronald Ngala.
Kulingana na mwalimu wa wakufunzi katika shirikisho la soka nchini Jones Kyalo anasema makocha wengi wamejitokeza kwa masomo hayo lakini wakalazimika kuwachukua 30 kuambatana na sheria za CAF.
Kocha Kyalo pia amewapongeza makocha wa shule za upili na msingi waliojitokeza kwa mafunzo hayo ya siku 10, akisema wakipata masomo mazuri watainua kiwango cha soka nchini.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































