MADAKTARI WAONYA DHIDI YA VITISHO KIAMBU

Muungano wa madaktari nchini KMPDU umeishutumu serikali ya kaunti ya Kiambu kutokana na vitisho vyake vya kuwafuta kazi madaktari wanaogoma, wakitaja hatua hiyo kuwa kinyume na sheria na ukiukaji wa haki zao.
Kwenye kikao na wanahabari, katibu mkuu wa muungano huo Dakta Davji Atellah, ametetea mgomo huo unaoendelea akisema unalindwa kisheria.
Madaktari kwenye kaunti hiyo wanalalamikia masuala kadhaa ikiwemo kuhamishwa kiholela.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa