#Local News

TULETEE MBOLEA KARIBU, WAKULIMA BUNGOMA

Wakulima wa mahindi katika kaunti ya Bungoma wameitaka serikali kuwasilisha mbolea ya ruzuku katika maeneo ya mashinani ikiwemo kwenye afisi za machifu badala ya maghala ya bodi za nafaka NCPB pekee, wakilalamikia mwendo mrefu wanaotembea kuchukua bidhaa hizo.

Wakizungumza na wanahabari katika eneo bunge la Webuye magharibi, wakulima hao wakiongozwa na Nancy Nelima wamesema umbali wa vituo hivyo umesababisha gharama ya ukulima kupanda.

Aidha, wameitaka serikali kuhakiki ubora wa mbolea hiyo kabla ya kuiwasilisha kwa wakulima.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

TULETEE MBOLEA KARIBU, WAKULIMA BUNGOMA

MGOMO: MATIBABU YALEMAZWA MTRH

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *