ALIYEKUWA GAVANA WA BUSIA SOSPETER OJAAMONG APATA KAZI KATIKA UTEUZI WA HIVI PUNDE WA RUTO
Rais William Ruto amefanya uteuzi mpya kwa mashirika mbalimbali ya serikali.
Katika notisi ya gazeti la serikali ya Juni 14, Ruto alimteua Aliyekuwa Gavana wa Busia Sospeter Odeke Ojaamong kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la NEPAD/APRM Kenya.
Ruto pia amemteua Bernadette Ng’ang’a kuwa mwenyekiti wa Baraza la Wahariri wa Kitabu cha Mwaka cha Kenya.
Ng’ang’a atakuwa mwenyekiti wa bodi hiyo kwa miaka mitatu kuanzia tarehe ya uteuzi.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































