KAMATI YA UTENDAJI YA AFC LEOPARDS YABUNI JOPO KAZI LA WATU WANNE

Mwenyekiti wa AFC Leopards Dan Shikanda amefichua kuwa Kamati ya Utendaji ya kitaifa ya klabu hiyo imebuni jopo kazi la watu wanane kubaini iwapo klabu hiyo inapaswa kubadilika kutoka katika mfumo wa kijamii hadi muundo wa ushirika.
Shikanda alisema kwamba kikosi kazi hicho kitaanza ziara ya kina ya matawi 85 ya klabu hiyo.
Shikanda pia alieleza kuwa kikosi kazi hicho kimepewa muda wa miezi sita ili kuhitimisha kazi yake na kuwasilisha matokeo kwenye kamati kuu.
Matokeo yamepangwa kutangazwa wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka ujao wa klabu.
Imetayarishwa na Janice Marete