ZIARA YA GACHAGUA BONDE LA UFA
Naibu Rais Rigathi Gachagua anatarajiwa kuanza ziara ya siku mbili katika eneo la Bonde la ufa huku kukiwa na minong’ono kuhusu kudorora kwa husiano baina yake na rais William Ruto.
Kwa mujibu wa ratiba, Gachagua anatarajiwa kuhutubia umma katika eneo la Silverline mjini Eldoret leo alasiri, huku akiwa mgeni wa heshima katika mkutano utakafanyika katika shule ya Seiyo eneo bunge la Keses hapo kesho.
Aidha, Gachagua atahudhuria kongamano la madhehebu mbali mbali eneo hilo siku ya Jumapili.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































