#Football #Sports

CLEOPHAS SHIMANYULA ANAAZIMIA KUNYAKUA WADHIFA WA MWENYEKITI WA FKF

Cleophas Shimanyula ambaye ni mwenyekiti na mwanzilishi wa klabu ya Kakamega Homeboyz, ni mmoja wa waaniaji wa Urais wa shirikisho la soka nchini FKF katika uchaguzi wa Disemba 7 mwaka huu.

Shimanyula meiongoza timu ya Homeboyz kutwaa kombe la FKF mwaka 2023 na pia ni mojawapo wa timu zinazofanya vyema katika ligi kuu ya Kenya.

Baadhi ya ajenda kuu kwenye manifesto yake Shimanyula ni kuweka mbinu mwafaka za kutafuta na kutambua talanta ili kuwa na timu za taifa bora,kushirikiana na serikali ili kuhakikisha upatikanaji wa raslimali za ujenzi wa viwanja vya kukuza soka tokea mashinani,na kuleta uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa kandanda.

Shimanyula pia amepata uungwaji mkono kutoka kwa mwakilishi wa zamani wa FKF magharibi ya Kenya, Andrew Amukowa.

aliibuni timu ya Homeboyz mwaka 2010 na miaka mitatu baadaye ikapandishwa ngazi kucheza Ligi kuu kwa mara ya kwanza mwaka 2013.

Homeboyz ilitwaa ubingwa wa kombe la FKF na kuiwakilisha Kenya katika kombe la shirikisho Afrika.

Imetayarishwa na Janice Marete

CLEOPHAS SHIMANYULA ANAAZIMIA KUNYAKUA WADHIFA WA MWENYEKITI WA FKF

POLISI LUGARI WACHUNGUZA KIFO CHA MKAZI ALIYEKUWA

CLEOPHAS SHIMANYULA ANAAZIMIA KUNYAKUA WADHIFA WA MWENYEKITI WA FKF

WASHUKIWA WATATU WA WIZI WAKAMATWA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *