MNATUMIWA VIBAYA, GACHAGUA AWAONYA WABUNGE
Aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua amewaonya wabunge kutoka eneo la Mlima Kenya wanaoegemea mrengo wa Rais William Ruto dhidi ya kile alichokitaja kuwa kutumiwa visivyo na Rais Ruto, akiwataka kuwa na msimamo na kupigania maslahi ya wakazi wa eneo hilo.
Gachagua amewahusisha wabunge hao na rabsha ambazo zimekuwa zikishuhudiwa kwenye mikutano yake, akiwatuhumu kwa kutumiwa na Rais Ruto kisiasa.
Aidha, amekosoa ombi la Rais Ruto kutaka asamehewe, akisema hilo pekee halitoshi bila fidia.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































