WAZIRI MVURIA KWA AFRIKA: TUONGOZE VITA DHIDI YA MABADILIKO YA HALI YA ANGA
Taifa la Kenya kupitia waziri Salim Mvuria imetoa changamoto kwa mataifa ya Afrika kuwa katika mstari wa mbele katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kuwekeza katika teknolojia ya kijani kibichi na nishati mbadala.
Waziri wa Uwekezaji, Biashara na Viwanda, Salim Mvurya, katika hotuba yake kwenye mkutano wa Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika (AfCFTA) mjini Kigali, Rwanda, amesema Afrika ina uwezo wa kuwa kinara wa kimataifa katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya muda mrefu ya hali ya anga.
Imetayarishwa na Mercy Asami
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































