MUGO SUPER CUP YATAMBA

Timu 41 zitamenyana kwenye mchuano wa Mugo Super Cup katika kaunti ya Lamu kikombe kilichodhaminiwa na mwenyekiti wa baraza la vyuma nchini ambaye pia ni kiongozi wa Lamu Francis Mugo.
Mwenyekiti wa ligi ya Mugo Super Cup Hussein Miji ameeleza kwamba timu hizo 41 kutoka wadi zote za Lamu zimelipa shilling elfu mbili kila timu ili kusajiliwa kujiunga kwenye mchuano huo.
Timu ya All Stars FC imeweza kumenyana na Golden Titas katika mchuano wa kufungua rasmi ligi hiyo katika uwanja wa Colombia Mokowe nakutoka sare tasa.
Imetayarishwa na Nelson Andati