GACHAGUA AJITENGA NA BAJETI YA 1.2B

Msimamizi wa mawasiliano katika afisi ya Naibu Rais Rigathi Gachagua, Njeri Rugene, amekanusha taarifa kwamba afisi ya Gachagua inapendekeza kutengewa kima cha shilingi bilioni 1.2 kwa ajili ya ukarabati katika mwaka ujao wa kifedha.
Katika taarifa hii leo, Rugene amevishutumu vyombo vya Habari kwa madai ya kutoa takwimu zisizo za kweli, na kuongeza kwamba afisi hiyo imependekeza shilingi milioni 300 kwa ukarabati na milioni 100 kwa ununuzi wa magari.
Taarifa yake hata hivyo inatofautiana na mwakilishi wa Gachagua aliyefika mbele ya kamati ya utawala na usalama katika Bunge la kitaifa kuwasilisha mapendekezo ya bajeti.
Imetayarishwa na: Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































