MKIMBIZI AJERUHI MKIMBIZI MWENZAKE HADI KUFA, HUKO KAKUMA
Mkimbizi amemvamia na kumuua mkimbizi mwenzake katika shambulizi jipya katika kambi ya Kakuma kaunti yaTurkana.
Hili ni shambulio la hivi punde zaidi kati ya wakimbizi katika kambi hiyo ambapo hadi wakimbizi 15 waliuawa katika mapigano kati ya koo mbili.
Kisa cha hivi punde kilitokea tarehe 11 katika kambi hiyo kubwa wakati mwanamume mmoja alipowashambulia watu wanne kwa kutumia panga.
Sababu ya shambulio hilo haijabainika ila inaaminika kuhusishwa na mapigano yanayoendelea huko.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 

























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































