#Local News

JUBILEE YATAKA EACC KUCHUNGUZA ‘WASHIRIKA’ WA ADANI

Chama cha Jubilee kimeitaka tume ya maadili na kupambana na ufisadi EACC kuwachunguza na kuwakamata maafisa wa serikali wanaohusika na mkataba baina ya serikali na kampuni ya Adani, siku moja baada ya kuibuka kwamba kampuni hiyo inakabaliwa na mashtaka ya ufisadi nchini Marekani.

Kupitia taarifa, katibu mkuu wa Jubilee Jeremiah Kioni amewataka maafisa wote husika kujiuzulu mara moja hadi uchunguzi dhidi yao utakapokamilika.

Huku akitilia shaka uamuzi wa Rais William Ruto kufutilia mbali mikataba katika sekta ya uchukuzi na kawi, Kioni amesema serikali ina mikataba Zaidi na Adani katika sekta ya afya, na kuwalaumu wabunge kwa kukosa kusimamisha mkataba huo bungeni.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

JUBILEE YATAKA EACC KUCHUNGUZA ‘WASHIRIKA’ WA ADANI

MWATSINGWA AIPA SS ASSAD USHINDI DHIDI YA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *