#Football #Sports

OTIENO AJIUNGA NA KINYANG’ANYIRO CHA URAIS WA FKF

Barry Otieno, katibu mkuu wa zamani wa Shirikisho la Soka la Kenya, atawania urais wa shirikisho hilo wakati wa uchaguzi wa kitaifa mwezi Desemba.

Otieno alijiuzulu kutoka wadhifa wa katibu wake wiki jana na kutangaza kuwania kwake jana Jumapili, siku moja kabla ya makataa ya kuwasilisha karatasi kwa Bodi ya Uchaguzi ya FKF.

Katika taarifa yake, alisema: “Dhamira na maono yake ni, kujenga taifa lenye nguvu zaidi, linalojumuisha watu wote na lenye mafanikio zaidi katika kandanda, kwa kuendeleza soka nje ya uwanja katika maeneo makuu manne: Uwezeshaji wa vilabu, uboreshaji wa utawala bora, maendeleo kamili na ngazi ya chini.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *