POLISI SIAYA WANACHUNGUZA KIFO CHA JAJI OGEMBO
Maafisa wa polisi kaunti ya Siaya wanachunguza kifo cha jaji msimamizi wa mahakama kuu ya siaya Daniel Ogembo ,baada ya kupatikana akiwa ameaga dunia ndani ya nyumba yake jana jumatano.
Mwili wa jaji Ogembo uligunduliwa na dereva wake alipofika nyumbani kwake kumchukua ili ampeleke kazini.
Kamanda wa polisi wa siaya Cleti Kimaoyo amesema uchunguzi umeanzishwa ili kubaini kilichosababisha kifo chake.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































