#Local News

POLISI UASIN GISHU ADAIWA KUWAUA WATU WAWILI

Maafisa wa polisi katika kaunti ya Uasin Gishu wanamzuilia mwenzao wa kituo cha Tembelio eneo bunge la Ainabkoi kwa tuhuma za kumpiga risasi hadi kufa mpenzi wake wa kike na mwanamme mwingine katika kinachoaminika kuwa mzozo wa kimapenzi.

Kulingana na kamanda wa polisi kaunti hiyo Benjamin Mwathi, tukio hilo lmefanyika usiku wa kuamkia leo katika eneo moja la burudani mtaani Jua Kali eneo la Turbo.

Ameongeza kuwa mwanamme huyo alijaribu kuingilia ugomvi kati ya mwathiriwa wa kike na mshukiwa, kabla ya mshukiwa kuwafyetulia risasi na kuwaua papo hapo.

Imetayrishwa na Antony Nyongesa

POLISI UASIN GISHU ADAIWA KUWAUA WATU WAWILI

RUTO AWAJIBU WANAOMTAKA AONDOKE

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *