MACHIFU MANDERA KUPEWA BUNDUKI, MURKOMEN

Serikali imetoa hakikisho la usalama katika eneo la Border One kwenye mpaka wa Kenya na Somalia baada ya kuibuka hofu mapema mwezi huu kuhusu uwepo wa vikosi vya wanajeshi wa Jubaland nchini Somalia.
Akizungumza alipozuru kaunti ya Mandera, Waziri wa usalama wa kitaifa Kipchumba Murkomen, amesema usalama wa ndani umerejeshwa na kwamba machafuko kwenye mataifa Jirani hayataathiri usalama nchini.
Amefichua kuwa machifu katika kaunti ya Mandera watapewa bunduki ili kuwalinda wananchi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa