RAIS RUTO ATANGAZA MIKAKATI YA KUIMARISHA UTALII
Ni afueni kwa sekta ya utalii baada ya serikali kuu kuimarisha juhudi za kuongeza idadi ya watalii wanaozuru taifa hili.
Ni taarifa ambayo ilitolewa na rais William Ruto akitaja kuwa lengo kuu ni kufikisha watali milioni tano wanaozuru nchi hii kufikia mwaka 2027.
Rais amesema kampeni hiyo inalenga kuitangaza Kenya kuwa nyumbani kwa kivutio muhimu ambacho ni bora kwa uvumbuzi, michezo, mikutano, wanyamapori na likizo.
Kiongozi wa taifa aliyasema hayo alipofungua rasmi maonyesho ya kuhama kwa Kongoni katika mbuga ya kitaifa ya Maasai Mara, kaunti ya Narok.
Zoezi hilo la kuhama kwa Kongoni huwavutia watalii wengi wa hapa nchini na kimataifa, huku hoteli zikijaa pomoni kwa lengo la kushuhudia tukio hilo la kustajabisha.
Kongoni hao huvuka mto Mara, katika vituo tofauti, huku mamba wakiwasubiri kwa hamu. Vita vya majini kati ya kongoni hao na mamba hupamba zoezi hilo, ambapo kila mtalii hujizatiti asipitwe na tukio hilo.
Imetayarishwa na Maureen Amwai
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































