ODINGA AWATAKA WABUNGE KUSALIMISHA NG-CDF, NGAF
Aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga ameendeleza shinikizo zake za kutaka kaunti kutengewa fedha zaidi, akiwataka wabunge kukabidhi hazina za NG-CDF na NGAF kwa magavana.
Akizungumza kwenye kongamano la ugatuzi linaloendelea katika kaunti ya Homa Bay, Odinga amezikosoa idara mbali mbali zilizo chini ya serikali kuu likiwemo bunge kwa madai ya kukwamia raslimali zinazofaa kusimamiwa na magavana.
Naye mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi, amezitaka kaunti kutumia raslimali inavyofaa huku akidai miradi yenye thamani ya shilingi bilioni 20 imekwama kutokana na matatizo ya mpito wa serikali.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































