RISING STARLETS WAINGIA AWAMU YA 3, KUMENYANA NA TANZANIA
Timu ya taifa ya soka kwa akina dada wasiozidi umri wa miaka 20 Rising Starlets wametinga awamu ya 3 kipute cha kufuzu kwa kombe la dunia baada ya kuwachabanga wenzao wa Ethiopia mabao 4-0 katika mkondo wa pili, na hivyo kufikisha jumla ya mabao 5-1.
Katika mechi ya marudiano hapo jana kwenye uwanja wa Ulinzi Sports Complex, Valary Nekesa aliwapa Ulinzi Starlets uongozi kunako dakika ya 4, kabla ya kufunga tena katika dakika ya 69, wafungaji wengine wakiwa Elizabeth Mideva na Fasila Adhiambo
Vipusa hao wa Kenya watamenyana na majirani Tanzania waliotandika Angola jumla ya mabao 7-0, kufuatia ushindi wa mabao 4:0 na mabao 3:0 katika mkondo wa kwanza na wa pili mtawalia.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































