UFICHUZI MPYA KWENYE KESI YA REX
Kesi kuhusu mauaji ya kijana Rex Maasai imechukua mwelekeo tofauti, baada ya mahakama kufahamishwa kwamba risasi iliyomwua haikufyetuliwa na bastola yoyote kati ya 3 zilizowasilishwa na mamlaka ya IPOA kwa uchunguzi katika maabara ya DCI.
Kulingana na mtaalamu wa udadisi wa silaha katika maabara ya DCI Alex Mwandawiro, hayo yameiweka kwenye njia panda ripoti iliyochukuliwa kama ushahidi katika kesi hiyo.
Aidha, ametofautiana na ripoti ya aliyekuwa kamanda wa polisi wa kituo cha Central Doris Mugambi kwamba risasi za raba pekee ndizo zilitumika katika maandamano.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































