TRAVERS AONDOKA BOURNEMOUTH
Everton ilimsajili kipa wa Ireland Mark Travers kutoka Bournemouth kwa mkataba wa thamani ya pauni milioni 4.
Travers alikubali kandarasi ya miaka minne na klabu hiyo ya Ligi Kuu, ambayo itafungua uwanja wao mpya mwanzoni mwa msimu ujao.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alisema anajivunia sana na anafurahi kuwa mchezaji wa Everton.
Travers, ambaye aliichezea Bournemouth mechi 82 katika kipindi cha miaka tisa akiwa na klabu hiyo, atachuana na kipa wa Uingereza Jordan Pickford kuwania nafasi ya kuanzia kwenye timu ya David Moyes.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 

















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































