#Sports

MAANDALIZI YA MAPEMA YALISAIDIA SOY UNITED KUPANDA DARAJA

Mwenyekiti wa Soy United Edwin Ayiro amehusisha kupandishwa daraja kwa timu hiyo kwenye Ligi Kuu ya Kitaifa (NSL) na maandalizi ya mapema na yaliyopangwa vyema.

Ayiro amrsema kupanga mapema kulichangia uchezaji wa kuvutia wa klabu hiyo msimu uliopita, na hatimaye kuipandisha daraja hadi NSL.

Amesema lengo la Soy tangu mwanzo lilikuwa ni kurejea ligi daraja la pili. Soy United ilicheza hapo awali NSL, na wanaporejea msimu ujao, Ayiro anasema wananuia kutumia mafunzo waliyopata kutokana na msururu wao wa awali, akitambua kuwa ligi imekuwa na ushindani zaidi.

Akitafakari kuhusu Ligi ya Daraja la Kwanza, Ayiro anasema ushindani ulikuwa mgumu, jambo ambalo liliwasukuma kufanya bidii zaidi, na hatimaye kuibuka mabingwa katika msimu uliomalizika hivi majuzi, kushindilia msumari wa mwisho wa NSL.

Imetayarishwa na Nelson Andati

MAANDALIZI YA MAPEMA YALISAIDIA SOY UNITED KUPANDA DARAJA

KIKOSI CHA KENYA TOKYO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *