#Local News

UGONJWA USIOJULIKANA MOMBASA WACHUNGUZWA

Wakenya na hasa wakaazi wa Mombasa wametakiwa kutokuwa na hofu serikali ikiendesha uchunguzi katika ugonjwa usiojulikana unaodaiwa kusababisha vifo vya watu 4 huko Migadini Mombasa.

Akiongea huko Kisumu mkurugenzi wa afya Dkt Patrick Amoth anasema uchunguzi wa awali umebaini kuwa waliofariki walikuwa pia wanaugua magonjwa mengine.

Naye waziri wa afya Aden Duale anasema chembe chembe kutoka kwa walioaga zinafanyikwa uchunguzi katika mahabara ya shirika la kemri huko Kilifi.

Imetayarishwa na Maureen Mukhobe

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *