JIANDAE KWA MVUA KUBWA, UTABIRI
Maeneo kadhaa nchini yametakiwa kujiandaa kwa vipindi vya mvua kubwa wiki hii huku maeneo mengi yakishuhudia vipindi vya ukame.
Katika ripoti yake kuhusu kipindi cha kati ya leo na Jumatatu wiki ijayo, idara ya utabiri wa hali ya anga imesema maeneo kama vile Nairobi, ukanda wa Ziwa Victoria, Rift Valley na Magharibi mwa nchi yatashuhudia mvua.
Aidha, baadhi ya maeneo hasa pwani yatashuhudia upepo mkali.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































