#Local News

Wabunge Nairobi wateta kuhusu uteuzi wa KDF

Jumla ya wabunge 18 kutoka kaunti ya Nairobi wamekosoa ratiba ya usajili wa makurutu wa kujiunga na jeshi la ulinzi KDF, wakisema ratiba hiyo inakiuka sheria kuhusu usawa na ujumuishaji jinsi ilivyo kwenye katiba.

Kupitia waraka, wabunge hao wamesema kuwa vituo 3 pekee vya usajili ambavyo ni uwanja wa Nyayo, Kasarani na jamhuri Grounds ni vichache ikilinganishwa na idadi kubwa ya jiji la Nairobi.

Sawa na ilivyo katika nyingi ya kaunti nchini, wabunge hao wametaka kila eneo bunge la jiji kutengewa kituo chake cha usajili.

Imeatayarishwa na Antony Nyongesa

Wabunge Nairobi wateta kuhusu uteuzi wa KDF

UASU, KUSU KIBABII WAGOMA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *