ACHA LALAMA MTOE SULUHU, SERIKALI
Viongozi wanaoegemea mrengo wa Kenya Kwanza wamewataka wenzao wa upinzani kusitisha shutuma dhidi ya serikali na badala yake kushirikiana ili kutatua changamoto zinazolikabili taifa.
Miongoni mwa viongozi hao ni naibu rais Kithure Kindiki, akizungumza kwenye kikao na mamia ya vijana nyumbani kwake katika kaunti ya Tharaka Nithi.
Kindiki amewahakikishia vijana kuwa serikali inaendelea na mikakati ya kupata suluhu kwa matatizo yanayowakumba vijana.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































