EGP AU MWONDOKE, RUTO
Wakati uo huo, mzozo kati ya baraza la magavana na serikali kuu kuhusu matumizi ya mfumo wa ununuzi wa kielekroniki umeendelea kutokota, Rais William Ruto akisisitiza kuwa mfumo huo utatekelezwa kwa lazima.
Akizungumza katika hafla ya kanisa kwenye kaunti ya Siaya, Rais Ruto amewataka maafisa wote wa ununuzi wanaopinga matumizi ya mfumo huo kujiuzulu.
Msimamo wa rais ukisisitizwa na viongozi waliokuwa wameandamana naye.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































