RAILA: NIKO NA RUTO HADI 2027
Nitamuunga mkono Rais William Ruto hadi akamilishe muda uliobaki wa muhula wake madarakani kufikia mwaka wa 2027.
Ni kauli ya kinara wa ODM Raila Odinga, akizungumza kwenye mahojiano na kituo kimoja cha runinga nchini ambako amesisitiza kuwa hakuna mazungumzo kati yake na chama cha UDA kuhusu uchaguzi mkuu ujao.
Amesema ushirikiano wake wa kisiasa na UDA ulilenga kumaliza taharuki nchini, na kuahidi kuwa waathiriwa wa maandamano wataanza kupewa fidia hivi karibuni.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































