MGOMO WA KIAMBU WAINGIA MAHAKAMANI
Mahakama ya uajiri na Leba imeizuia serikali ya kaunti ya Kiambu kuwaajiri madaktari wapya hadi mgomo unaoendelea wa madaktari utakaposuluhishwa.
Katika maagizo ya muda yaliyotolewa na jaji Njagi Marete, serikali hiyo imetakiwa kutatua malalamishi yaliyoibuliwa na madaktari walio kwenye mgomo na kupata suluhu kwa mvutano kati yake na madaktari hao.
Kesi hiyo iliyowasilishwa na muungano wa madaktari KMPDU kupinga tangazo la kuwaajiri madaktari 78, itaanza kusikilizwa tarehe 28 mwezi huu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































