#Local News

HOJA YA MUTAI KUENDELEA SENETI

Vikao vya kusikiliza hoja ya kubanduliwa kwa gavana wa Kericho Erick Mutai kutoka mamlakani vinaingia siku ya pili hii leo katika bunge la seneti baada ya kuanza hapo jana ambapo gavana huyo alidai mchakato wa kumbandua ulichochewa kisiasa.

Kulingana na gavana huyo kupitia kwa mawakili wake, spika wa bunge la kaunti hiyo alianzisha mchakato huo kwa malengo yake ya kibinafsi ikiwemo azma yake ya kuwania wadhifa wa ugavana katika siku zijazo.

Hata hivyo, mawakili wa bunge hilo wakiongozwa na Elisha Ongoya, wameshikilia kuwa tuhuma zilizoibuliwa dhidi ya gavana huyo zina uzito na hivyo zinafaa kuzingatiwa na maseneta.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

HOJA YA MUTAI KUENDELEA SENETI

VUTA VUTA ZA SHA ZAINGIA SIASA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *