MALENGO YA IEBC KABLA YA 2027
Zoezi la kuwasajili wapiga kura wapya limeingia siku ya pili hii leo, tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC ikisema inalenga kufikisha wapiga kura milioni 28.5 kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 kutoka milioni 22.1 wa sasa.
Mwenyekiti wa IEBC Erastus Ethekon, amesema wanalenga kuwasajili wakenya walio na umri wa miaka 18 au zaidi na ambao hawajawahi kusajiliwa.
Aidha, wanaotaka kubadilisha vituo vya kupigia kura pia watapata fursa kwenye zoezi hilo la kitaifa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































