#Local News

UPINZANI KUZINDUA JINA, NEMBO WIKI IJAYO

Muungano wa upinzani ukiongozwa na aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua na kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka umeratibiwa kuzindua jina lake rasmi na nembo Jumatatu wiki ijayo katika maandalizi ya chaguzi ndogo zijazo na uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Uzinduzi huo hata hivyo unajiri huku migawanyiko ikishuhudiwa kwenye muungano huo kuhusiana na uteuzi wa Waziri wa zamani Mukhisa Kituyi kuwa msemaji wake.

Kulingana na naibu kinara wa DCP Cleophas Malala, muungano huo unahitaji msemaji mwenye uwezo wa kushirikiana na uongozi wa vijana ili kuleta mageuzi katika siasa za humu nchini.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

UPINZANI KUZINDUA JINA, NEMBO WIKI IJAYO

OPERESHENI MAALUM YAAGIZWA JIJINI

UPINZANI KUZINDUA JINA, NEMBO WIKI IJAYO

WANAJESHI WAKOSESHA UTULIVU MANDERA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *