#Business

WAKENYA WAONYWA KUJIANDAA KUHUSU SUKARI GHALI

Wakenya wameonywa kuhusu uwezekano wa kupanda kwa bei ya sukari huku sekta ya sukari nchini ikikabiliwa na kudorora upya.

Utafiti wa Julai 2025 wa Benki Kuu ya Kenya (CBK) unaonyesha kuwa wateja wanatarajia bei kupanda zaidi kutokana na kufungwa kwa viwanda, kuporomoka kwa utoaji wa miwa, na kutokuwa na uhakika kuhusiana na ukodishaji wa viwanda vya sukari kwa wahudumu wa kibinafsi.

Licha ya kuimarika kwa usambazaji wa vyakula vingine vikuu, bei ya sukari inaendelea kupanda. Uzalishaji wa miwa ulipungua hadi tani 383,050 mwezi Mei kwa miezi 18, wakati uzalishaji wa sukari ulishuka hadi tani 32,760, kiwango cha chini zaidi tangu Novemba 2023.

Imetayarishwa na Maureen Amwayi

WAKENYA WAONYWA KUJIANDAA KUHUSU SUKARI GHALI

CHAN YAINGIA NUSU FAINALI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *