KILIO CHA WAFANYABIASHARA TOI
Wafanyibiashara wa mitumba katika soko la Toi, mtaani Kibera, jijini Nairobi wameibua wasiwasi kuhusu hasara wanayopata kutokana na kodi wanaotozwa kila wakati wanaponunua bidhaa.
Wamelalamika madai ya kunyanyaswa mara kwa mara na maafisa kutoka katika
serikali ya kaunti ya Nairobi, hali wanayosema imechangia wenzao kuacha
biashara.
Hata hivyo, wakiongozwa na Philp Wambua, wamelalamikia changamoto zikiwemo viwango vya juu vya kodi, mazingira mabovu ya kazi na ukosefu wa taa za barabarani.
Aidha, wafanyabiashara hao wamelazimika kuongeza bei kwa bidhaa zao, hali
wanayosema imepunguza mauzo kutokana mapato ya chini ya wanunuzi.
Sasa wameitaka serikali kuu kuboresha uchumi, mbali na kuimarisha usafi wa mazingira usalama katika soko hilo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































