OJAL ANASEMA WAKO TAYARI KUTETEA TAJI LAO
Kocha wa timu ya Rugby 7s Strathmore Leos, Willis Ojal amesema kuwa timu hiyo iko tayari katika kinyang’anyiro cha Prinsloo 7s wikendi hii huko Nakuru na lengo lao ni kutetea taji lao la mwaka jana.
Leos wikendi iliyopita wameongoza katika finali iliyochacha ya Driftwood 7s dhidi ya KCB katika Kaunti ya Mombasa na sasa wanasafiri kuelekea kwa mashindano hayo ya Prinsloo.
Leos watakuwa katika kitengo cha B ambapo watamenyana na Menengai Oilers, Daystar Falcons na mabingwa wa kitengo cha pili katika Driftwood 7s, Zetech Oaks.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































