#Sports

TUZO, FEDHA ZA MOROCCO CHAN

Timu ya soka ya taifa Morocco imetia kibindoni kima cha shilingi milioni 455 baada ya kuvikwa taji la 3 ya ubingwa wa mashindano ya mataifa bingwa barani Afrika kwa wachezaji wa ligi za nyumbani CHAN yaliyokamilika Jumamosi usiku.

The Atlas Lions waliibuka mabingwa wa mashindano hayo baada ya kuwacharza Madagascar mabao 3:2 na kuwanyima fursa ya kuwa Kisiwa cha kwanza au time ya Kusini mwa Afrika kuwa buingwa wa CHAN

Ushindi huo wa Morocco sasa umeashiria mwisho wa mashindano ya CHAN 2024 na sasa macho yanaelekezwa kwa kombe la AFCON litakaloandaliwa mwaka 2027 huku Kenya, Uganda na Tanzania wakiwa wenyeji wa mashindano hayo.

Wakati uo huo, Morocco walitamalaki tuzo za mashindano hayo kwa wachezaji binafsi.

Mohamed Rabbie Hrimat alikuwa mchezaji bora wa michuano hiyo, huku mwenzake Oussama Lamlaoui akiwa mfungaji bora baada ya kufunga mabao sita na golikipa wa senegal Marc Diouf akitawazwa golikipa bora wa michuano ya CHAN.

Senegal pia walitawazwa kama timu iliyokuwa na nidhamu nzuri katika mechi zao.

Imetayarishwa na Nelson Andati

TUZO, FEDHA ZA MOROCCO CHAN

IKULU KITOVU CHA UFISADI- GACHAGUA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *