#Business

Kizungumkuti cha ukaguzi

Mdhibiti wa Bajeti Margaret Nyakang’o amefichua kuwa afisi yake haiwezi kutekeleza majukumu ya uangalizi wa bajeti na matumizi ya pesa zinazokusanywa kwa Ushuru wa Nyumba, ambayo inakadiriwa kuwa shilingi bilioni 63 kila mwaka.

Katika ripoti ya Kamati ya Bunge ya Kusimamia Utekelezaji Katiba, Nyakang’o ameeleza kuwa mfuko huo umeainishwa kuwa ni Tozo, hivyo haujapangiwa bajeti na kusema kuwa kodi iko nje ya mamlaka ya ofisi yake.

Kufuatia mwanya huo wa kisheria, wabunge wanataka kuifanyia marekebisho sheria hiyo, ambayo fedha zote maalum na tozo zitafuatiliwa na CoB.

Ushuru wa Makazi ulianzishwa katika Mswada wa Fedha wa 2023. Baada ya kuanzishwa kwake, Wakenya wanaolipwa mishahara hulipa ushuru wa 1.5% kwa ushuru unaofadhili mradi wa Nyumba Nafuu kote nchini.

Imetayarishwa na Maureen Amwayi

Kizungumkuti cha ukaguzi

KENYA AIRWAYS YAJIPIGIA DEBE

Kizungumkuti cha ukaguzi

OUMA NJE YA KIKOSI CHA MCCARTHY

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *