MANCHESTER UNITED WAJIPANGA KWA MSIMU MPYA
Manchester United wanatazamia kurejea msimu huu kwa kishindo ni baada ya kumaliza vibaya zaidi kuwahi kutokea katika Premier League.
United walimaliza katika nafasi ya 15 msimu uliopita na kushindwa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa baada ya kupoteza fainali ya Ligi ya Europa dhidi ya Tottenham.
Tayari wameimarisha kikosi chao kwa kuwaongeza Bryan Mbeumo, Matheus Cunha na Diego Leon, huku Marcus Rashford akijiunga na Barcelona kwa mkopo na Christian Eriksen na Victor Lindelof wametolewa. mwenzake Lois Openda hatahamia Sunderland.
United na Newcastle zote zina nia ya kumsajili Sesko, ambaye alifunga mabao 21 katika michezo 45 katika michuano yote msimu uliopita.
Mshambulizi mwenza wa Leipzig Openda alikuwa anahusishwa sana na Sunderland na hakuna uwezekano wangewaacha washambuliaji wawili kuondoka kwenye dirisha moja.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































