AFISA ALIYEFARIKI HAITI KUWASILISHWA NCHINI
Familia ya afisa wa polisi Kennedy Mutuku aliyefariki kwenye ajali nchini Haiti inatarajiwa kupokezwa mwili wa afisa huyo utapowasilishwa nchini hii leo kutoka Haiti.
Kulingana na idara ya polisi, Mutuku mwenye umri wa miaka 41, alikuwa akihudumu katika kitengo cha RDU, na alifariki baada ya gari lao lilolokuwa likikokotwa kupata matatizo ya kiufundi kabla ya kugongwa mnamo tarehe 31 mwezi jana.
Mutuku ni afisa wa 3 ambaye amethibitishwa kufariki nchini humo, mwingine akiwa Benedict Kabiru ambaye kulingana na Waziri wa usalama Kipchumba Murkomen, polisi walichelewa kuifahamisha familia kuhusu kifo chake kilichowekwa wazi na Rais William Ruto.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































