#Sports

CAF: POLICE FC WAWATIA PINGU WAGENI, NAIBOIS WAAMBULIA SARE

Mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini KPL Kenya Police wameanzisha kampeni yao ya kusaka ubingwa wa bara Afrika kwa ushindi mnono wa mabao 3:1 dhidi ya Mogadishu City Stars wa Somalia katika mkondo wa kwanza kwenye mashindano ya klabu bingwa barani Afrika CAF Championship.

Maafande hao ambao wanashiriki mashindano ya bara kwa msimu wa 2 baada ya kushiriki mashindano ya CAF Confederations msimu jana ambako walibanduliwa katika raundi ya kwanza, walianza mechi hiyo ya Jumamosi kwa kishindo na kuchukua uongozi katika dakika ya 15 kupitia kwa Eric Zakayo.

Hata hivyo, mabingwa wa Somalia walisawazisha mambo baada ya mapumziko, ila Police FC wakatia pingu Mogadishu Stars kupitia kwa Edward Omondi na David Simiyu.

Akizungumza baada ya mechi hiyo, kocha mkuu wa Police FC Etienne Ndayiragije aliwamiminia sifa vijana wake, akisema walistahili kupata ushindi mnono zaidi yah apo.

Huku hayo yakijiri, Nairobi United walilazimisha sare ya mabao 2 dhidi ya NEC FC wa Uganda kwenye awamu sawa kwenye mashindano ya CAF Confederation Cup dakika za lala salama.

Licha ya uongozi wa mapema, Naibois walijikuta nyuma ya wenyeji wao kunako dakika ya 80, ambao pia walipewa mkwaju wa penalti katika dakika ya 90.

Hata hivyo, nguvu mpya Shami Kibwana aliwapa Naibois afueni kwa kulazmisha sare katika mechi hiyo, wanapojiandaa kwa marudiano tarehe 27 jijini Nairobi.

Imetayarishwa na Nelson Andati

CAF: POLICE FC WAWATIA PINGU WAGENI, NAIBOIS WAAMBULIA SARE

WANARIADHA WA KENYA WATIA FORA WAC

CAF: POLICE FC WAWATIA PINGU WAGENI, NAIBOIS WAAMBULIA SARE

SHABANA FC WAANZA LIGI KWA KISHINDO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *